picha ya mto Naili
Wananchi mkoani Njombe wametakiwa kutunza mazingira na vyanzo vya maji kwa kuto kujihusisha na shughuli za kilimo karibu na vyanzo vya maji kwani shughuri hizo ndio chanzo kikubwa cha uharibifu na ukaushaji wa vyanzo vya maji.
Wito huo umetolewa na mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Njombe DAUDI MAJANI , katika mazungumzo yake na waandishi wa habari kwa lengo la kutaka kufahamu namna ambavyo mkoa umejipanga kukabiliana na changamoto za utunzaji wa mazingira kwa manufaa ya jamii na kizazi kijacho.
Majani amesema kuwa kwa sasa wananchi wamekuwa na hamasa kubwa katika upandaji wa miti zoezi ambalo litasaidia kutunza vyanzo vya maji na kuitaka jamii kuwa na uelewa kuhusu miti na vyanzo vya maji pamoja na kujua umbali kutoka mpaka wa chanzo cha maji mpaka mche wa mti ulipo.
Tamko hilo limekuja kufuatia taifa la Tanzania kuazimisha siku ya Mto Nile ambapo maadhimisho hayo kitaifa yamefanyika Mkoani Dar es salaam nchini hapa hivyo ili kuunga mkoano maadhimisho hayo Mkurugenzi mtendaji wa maji safi na Usafi wa mazingira amewataka wananchi kutunza vyanzo vya maji.
Ni lazima tutunze vyanzo vya maji kwa manufaa ya jamii na kizazi kijacho
-
0 comments:
Post a Comment