Na:Amiri kilagalila
Ili kuendeleza jitihada za kukuza kiwango cha elimu mkoani Njombe serikali imeendelea kuonyesha juhudi katika kukuza kiwango cha taalumu, zoezi hilo limeendelea kupewa nguvu na baadhi ya shule pamoja na vituo vya elimu ambapo hii leo kumekuwa na majadiliano kwa wanafunzi wa kituo cha mafunzo cha enhancement education centre, wanafunzi wamechanganua maada "je ujio wa wakoloni ulipelekea maendeleo Afrika?"
Mjadala huo umewakutanisha wanafunzi wa kidato cha kwanza pamoja na cha nne ambapo kidato cha pili wakiungana na kidato cha tatu kukubali hoja, Umahili mkubwa umeendelea kuonekana kwa wanafunzi wote katika kujenga hoja kwa pamoja. pongezi za dhati sana kwa wanafunzi wote walio jaribu kuonesha nia katika kutafuta elimu.
Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher olesendeka aliwahi kuzipongeza shule mbali mbali mkoani kwa ufaulu mzuri wakidato cha nne mwaka 2017 na kuzitaka shule zote kuungana kwa pamoja ili kuonyesha uwezo kitaifa zaidi ya mwaka 2017.
0 comments:
Post a Comment