Mzee wa upako ameyasema hayo alipotafutwa na E-News ya EATV baada ya kuulizwa maswali juu ya kauli hiyo.
“Kama
unakuja kanisani kwa maana kuna biashara, nakupa miaka hii mitatu sio
utatembelea ndala utatembelea kucha, ni mtoto mdogo sana hana akili.
"Mungu
hataniwi, anafanya kufuru, kama ana mama yake amemzaa amuonye. Mimi
biblia nimesoma na hizo lugha zake nyepesi zitamtokea puani, asithubutu
kufanya kanisa kama biashara.
"Baada
ya miaka hii mitatu atajua kwamba kuongoza watu sio kama kuongoza
ngo’mbe hakuna jambo gumu kama kuongoza watu wenye akili kama wewe wenye
ufahamu kama wewe, wapo watu wengi walianzisha makanisa kwanini
walifunga, ujinga hujui ni ujinga ni utoto,” alisema Mzee wa Upako.
0 comments:
Post a Comment