internet advertising Boda boda waandamana mkoani Njombe,waitaka Sumatra kuziachia piki piki zilizokamatwa | DotFIVE

Boda boda waandamana mkoani Njombe,waitaka Sumatra kuziachia piki piki zilizokamatwa

    Boda boda wakikusanyika ofisi za ujenzi halmashauri ya mji wa Njombe
    Na:Amiri kilagalila
 Madereva wa bodaboda mkoani njombe wameandamana hadi ofisi za ujenzi halmashauri ya mji wa       Njombe wakiwa na madai ya kutolewa kwa piki piki tatu zilizokamatwa na mamlaka ya usafirishaji SUMATRA katika kijiwe cha standi na kuhifadhiwa katika ofisi hizo.


 Kufuatia maandamano hayo baadhi ya viongozi wa bodaboda ambao walifika na kuzungumza na Mamlaka ya usafirishaji SUMATRA wamesema kuwa mamlaka hiyo imechukuwa uamuzi wa kukamata pikipiki hizo hii leo ikiwa ni siku ya mwisho tangu kutolewa kwa maagizo ya mkuu wa wilaya kuwataka madereva wote kuwa na leseni za biashara pamoja na stika na kukubaliana kupunguza kodi hizo huku akiongeza kuwa hawatatoza kodi mpaka watakapo fikia makubaliano katika kikao kitakacho husisha uongozi wa mkoa na viongozi wa usalama barabarani kitakachofanyika tar.24 mwezi wa pili ili kufikia maamuzi juu ya mlundikano wa kodi hizo.

Aidha madereva hao wameeleza kuwa hatua ya ukamataji iliyofanywa na mamlaka hiyo si sahihi kwani wamekamata pikipiki hizo zikiwMadereva hao wamebainisha sababu nyingine ilyopelekea wao kuchukua uamuzi wa kufanya maandamano kuwa ni kitendo cha halmashauri kuchukua kodi mbili kwa madereva hao hali ambayo inaumiza kiuchumi.a zimepakiwa bila kuwashirikisha  wamiliki wa pikipiki hizo.

Katika hatua nyingine Madereva hao wamesema kuwa hawapotayari kulipa mpaka mkuu wa wilaya atakapo itisha kikao na ili kufikia makubaliano ya maandishi na madereva hao ndipo wataanza kulipia kodi hizo.


Baadhi ya viongozi waliofika katika ofisi za sumatra wamesema kuwa wamekubaliana kutokamatwa na sumatra hadi tarehe ishirini na nne siku ambayo kikao kitafanyika huku akiongeza sumatra wamewataka kulipia pikipiki zilizokamatwa hali ambayo imepingwa na madereva hao.

    Viongozi wa boda boda wakizungumza na baadhi ya madereva

Ni siku chache zimepita tangu mkuu wa wilaya ya njoimbe Ruth msafiri kuitisha kikao cha Viongozi wa madereva wa Bodaboda kikao ambacho kilishindwa kufikia muafaka baada ya viongozi hao kushindwa kuafiki maamuzi ambayo mkuu wa wilaya aliyatoa juu ya kikao hicho lakini majibu juu ya mlundikano wa kodi huenda yakapatikana siku ya tarehe 24 baada ya kufanyika kika kati ya uongozi wa mkoa na usalama barabarani  pamoja na madereva hao.


Share on Google Plus

About Amiri kilagalila

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment