Serikali
imewataka wananchi kuanzisha desturi ya kununua kazi za wasanii,
kwakuwa ndiyo njia pekee inayoweza kuwanufaisha kwa kazi wanazozifanya.
Wito
huo umetolewa wiki hii na Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni
na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel wakati akizungumza kwenye uzinduzi
wa tovuti a Afro Premiere, iliyoanzishwa kwa lengo la kuuza video za
muziki za wasanii.
Alisema
mpango huo unaweza kuwa ni moja ya mikakati muhimu ya kupambana na wezi
wa kazi za wasanii, kwakuwa video za muziki zitakuwa zikipatikana
kwenye mtandao huo peke yake kwa kipindi maalum na hivyo kuingiza pesa
zinazoenda kwa msanii, serikali na watayarishaji moja kwa moja.
Pia
alidai kuwa kwakuwa Afro Premiere itakuwa ikiweka nyimbo za Kiswahili
zaidi, itasaidia kukikuza zaidi Kiswahili, ambacho ni cha 10 kati ya
lugha elfu sita duniani na kuahidi kupitia wizara ya mambo ya nje,
wizara yake itawaunganisha na Watanzania waliopo nje ya nchi.
Prof Ole Gabriel amewataka wasanii wao wenyewe kuunga mkono mpango huo sababu ndio njia pekee ya kuufanya ufanikiwe.
“Mpango
huu utafanikiwa kama ninyi mkiwa sehemu ya mpango huu, kama ninyi
wenyewe tena mkianza kuwa na kona kona na kuupiga vita, basi mpango huu
utaonekana feki na utashindikana,” alisema.
Hadi
sasa kuna video mbili mpya zilizowekwa kwenye Afro Premiere ambazo ni
Go Low ya G-Nako na Jux pamoja na K wa Roma na Baghdad. Mashabiki
wanaweza kununua nyimbo hizo kwa shilingi 300 tu kwa kutumia simu zao.
0 comments:
Post a Comment