Rais
wa Marekani, Donald Trump ametangaza kuwa anataka kujenga kinu kikubwa
cha nyuklia nchini humo kuhakikisha kuwa taifa hilo lenye nguvu zaidi
duniani linaendelea kuwa juu zaidi katika silaha za nyuklia.
Akizungumza
leo katika mahojiano maalum na shirika la habari la Reuters, Rais Trump
amesema kuwa Marekani sasa hivi iko nyuma katika uwezo wake wa silaha
za atomiki.
Katika
hatua nyingine, Reuters imemnukuu Trump akizungumza baada ya mahojiano
hayo, ambapo alieleza kuwa anachukizwa sana na kitendo cha Korea
Kaskazini kufanya majaribio ya silaha zake za maangamizi.
Alisema kuwa katika kuidhibiti Korea Kaskazini, Marekani inapaswa kutumia mfumo wa nchi marafiki kama Japani na Korea Kusini.
Ni
nchi tisa pekee duniani zilizothibitisha kuwa na silaha za kinyuklia
ambazo ni Urusi, Marekani, China, India, Israel, Ufaransa, Korea
Kaskazini, Pakistan na Uingereza. Nchi nyingine zinazodaiwa kuwa na
silaha hizo zimekua zikikanusha vikali na kudai kuwa zinatumia nyuklia
kama nishati.
Kwa
mujibu wa shirika linalojihusisha na masuala ya usalama, Ploughshares
Fund, linakadiria kuwa kuna zaidi ya silaha za nyuklia 15,000 duniani
kote, ambapo Marekani na Urusi pekee zinamiliki zaidi ya asilimia 93 ya
silaha hizo.
0 comments:
Post a Comment