prof. Mohamed janab
Na:Amiri kilagalila
Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya jakaya kikwete prof.janab amesema kuwa taasisi hiyo licha ya kuonyesha umahili katika ufanyaji kazi na kufanikiwa kutoa huduma ya magonjwa makubwa ambayo yameshindikana katika hospitali zingine,
Kituo kimeendelea kukumbana na changamoto ya kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa wanaofika katika kituo hicho lakini baado panakuwa na upungufu wa watumishi wa kutosha,
"Wagonjwa wengi sana wapo wanaletwa katika kituo chetu kutoka muhimbili na sehemu zingine lakini sisi pale wafanyakazi ni wachache kwa hiyo bado hiyo ni changamoto kwetu" Janab amesema
Katika hatua nyingine mkurugenzi huyo amesema kuwa ipo changamoto ya tatizo la umeme ambapo amesema licha ya kuwa na jenereta lakini nishati hiyo sio nzuri katika matumizi ya kituo kwa kuwa huwezi kutumia jenereta wakati wote kwa kuwa hiyo ni emergence,ameiomba serikali kuangali namna ya kutenga kiasi cha umeme maalumu unaoweza kutumika katika tasisi kama hizo ili kuondokana na tatizo la kukatika kwa umeme ili kazi iweze kufanyika kwa ufasaha.
Pia amesema kuwa wakati mwingine hukabiliwa na changamoto ya ukosefu wa damu husasani kwa wagonjwa wa upasuaji na wakati damu inapohitajika kwa kuwa ni muhimu katika vituo kama hivyo damu iwepo wakati wote ili kuokoa maisha ya wahitaji,
Aidha akizungumza kipindi cha dakika 45 kinacho lushwa na kituo cha ITV kila jumatatu profesa Janab amesema kuwa serikali imekuwa mstari wa mbele kuondoa kodi na kuhakikisha wagonjwa wote walio kuwa wanakwenda Nje ya nchi kwa sasa wanaletwa katika kituo hicho ambapo ni hatua kubwa ya kihuduma Nchini Tanzana na kuzipongeza pia sekta binafsi kwa kuwa zimesaidia sana katika kuendeleza shughuli za tasisi hiyo.
Tunafanya kazi kwa ufanisi lakini zipi changamoto katika taasisi ya moyo ya jakaya kikwete
-
0 comments:
Post a Comment