internet advertising SHULE YA MSINGI LUHUJI MKOANI NJOMBE YAPOKEA MSAADA WA MIFUKO 20 YA SIMENT | DotFIVE

SHULE YA MSINGI LUHUJI MKOANI NJOMBE YAPOKEA MSAADA WA MIFUKO 20 YA SIMENT

   Wanafunzi wakishusha mifuko ya siment
   Na:Amiri kilagalila

Diwani wa viti maalum mkoani Njombe jimbo la Njombe mjini  kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi CCM ANGELA MWANGENI ametoa msaada wa mifuko ishirini ya simenti kwa ajili ya ujenzi wa jiko katika shule hiyo ili kufanikiwa kutatua baadhi ya changamoto zilizopo shuleni hapo.

Diwani viti maalumu bi.ANGELA MWANGENI wa kwanza kushoto akizungumza na badhi ya watu alio    ongozana nao katika shule hiyo.

Mwangeni ametumia fursa hiyo kuwasihi madiwani wenzake wa viti maalum kutumia nafasi waliyo nayo ili kutatua changamoto mbali mbali zilizopo katika shule hiyo ili wanafunzi waweze kusoma katika mazingira rafiki na kuboresha taaluma yao, katika hatua nyingine amesema kuwa msaada huo alio utoa hauwezi kumaliza tatizo shuleni hapo zaaidi ya kupunguza kidoga hivyo na wajibu wa kila kiongozi kuhakikisha anafanya hivyo kwa maslahi ya Taifa kwa ujumla.

Mtunza stoo wa shule pamoja na wanafunzi wakihesabu mifuko ya simenti

Naye mwalimu mkuu wa shule hiyo bi.ADELHELMA MAPUNDA amemshukuru diwani huyo kwa msaada huo na kumpongeza kwa uzalendo aliouonesha katika shule yake licha ya kuwepo kwa shule nyingi ambazo angeweza kupeleka msaada huo, na kuwaasa wazazi  kuendelea kuchangia ujenzi wa madarasa na kutoa michango mingine kama ya chakula kwa ustawi wa wanafunzi.
Share on Google Plus

About Amiri kilagalila

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment