Home / Uncategories / Samson na Ndoto Za Kuzinoa Afrika Kusini, Rwanda
Samson na Ndoto Za Kuzinoa Afrika Kusini, Rwanda
-
By
Ghation Sports
Gwiji wa soka nchini Nigeria Samson Siasia ameonyesha dhamira ya
kurejea kwenye ukufunzi wa mchezo huo barani Afrika, kufuatia mataifa
kadhaa kusaka makocha watakao kabidhiwa jukumu la kufuzu fainali za
kombe la dunia 2018 na zile za AFCON za mwaka 2019.
Siasia ambaye amekua nje ya ukufunzi wa soka tangu alipoachana na
kikosi cha timu ya taifa ya Nigeria chini ya umri wa miaka 23
kilichotwaa medali ya shaba ya fedha wakati wa michuano ya Olimpiki ya
mwaka 2016, juma lililopita alitajwa kuwa sehemu ya makocha 52 walioomba
kazi ya kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya Rwanda.
Jina la kocha huyo pia limejitokeza katika orodha ya watu wanaowania
nafasi ya kukinoa kikosi timu ya taifa ya Afrika kusini ambacho kwa sasa
hakina kocha mkuu, baada ya kutimuliwa kwa Ephraim Mashaba tangu mwezi
Disemba mwaka jana.
Mpaka sasa makocha 32 wameshawasilisha maombi ya kuwania ukuu wa kiti cha benchi la ufundi la Afrika kusini.
Jina lingine ambalo limeonekana kwenye orodha hiyo ni la aliekua
meneja wa klabu ya Man City, Inter Milan na Galatasaray Roberto
Mancini, aliyekua kocha mkuu wa timu ya taifa ya Italia Giovanni
Trapattoni pamoja na Hassan Shehata ambaye alikisaidia kikosi cha Misri
kutwaa ubingwa wa AFCON mwaka 2006, 2008 na 2010.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment