Madereva boda boda wakitawanyika eneo la kikao
NA:Amiri kilagalila
Hali hiyo imetokea hii leo baada ya mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth msafili kutoa maagizo ya maridhiano ya awali kuwa ifikapo hii leo tarehe kumi na sita ya mwezi wa pili ni lazima kila dereva boda boda kuhakikisha anakuwa na leseni ya biashara pamoja na kusajili stika kwa hiari, Hatua hiyo ni kutokana na makubaliano ya kikao kilichofanyika mwezi wa kwanza mwaka huu ili kuhakikisha kila boda boda analipa mapato kutokana huduma hiyo.
kikao hicho kilichoitishwa katika ofisi ya mkuu wa wilaya kimekutanishA viongozi mbali mbali wa boda boda kutoka halmashauri ya mji mdgo wa makambako, viongozi wa boda boda halmashauri ya mji wa Njombe,Afisa mfawidhi sumatra mkoa wa Njombe na viongozi wengine wa serikali kimekuwa na lengo la kutoa maagizo ya utekelezaji kutokana na makubaliano ya awali.
Mkuu wa wilaya ya Njombe akizungumza jambo.
Katika hatua nyngine msafiri ameongeza siku 3 kwa maafisa usafilishaji abilia haoili kuhakikisha kwa wote waliobakia kusajili biashara zao wanatekeleza agizo hilo kwa kuwa siku walizokubaliana awali zimekwisha hii leo, pia ameongeza kusema kuwa baada ya siku hizo tatu kufika maafisa wa sumatra na jeshi la polisi watakuwa mtaani ili kuwabaini walio kiuka maagizo hayo.
MADEREVA BODA BODA WAMESHINDWA KUFIKIA MAKUBALIANO NA DC NJOMBE
-


0 comments:
Post a Comment