Waziri wa mambo ya ndani Mwigulu lameck Nchema ameliagiza jeshi la polisi nchini kuendelea kuongeza nguvu na kutumia jitiada zote ili kuhakikisha linapambana na watu wanao jihusisha na usambazaji pamoja na uuzaji wa madawa ya kulevya nchini ili kusaidi jamii hususani vijana ambao kwa kiasi kikubwa wamekuwa wakiathiriwa na matumizi ya madawa ya kulevya.
Nchemba ameyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na jeshi la polisi mkoani NJOMBE katika ukumbi wa chuo cha maendeleo ya wananchi Njombe, ikiwa ni ziara yake ya kwanza mkoani humo, wakati akiendelea na ziara katika mikoa mbali mbali hapa nchini ili kutathmini jitihada na kazi za jeshi la polisi
.
Maafisa wa jeshi la polisi wakisikiza maelekezo
Katika hatua nyingine waziri wa mambo ya ndani amelitaka jeshi la magereza kutumia nguvu kazi iliyopo katika uzalishaji ili kusaidia upungufu wa chakula, Nchemba amesema kuwa jeshi la mageleza linapaswa kuwatumia wafungwa wanaotumikia adhabu zao katika shughuli za kilimo ili kupata cha kutosha na kuweza kulisha sehemu zenye uhitaji.
Kabla ya kukutana na jesi hilo la polisi katika halmashauri ya mji wa Njombe alitembelea kikosi cha jeshi namba 514 KJ kilichopo wilaya ya kipolisi katika mji mdogo wa Makambo na kushiriki zoezi la upandaji miti ili kuunga mkono jitihada za mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher olesendeka katika kampeni yake ya upandaji miti ya vivuli,maua na matunda ili kuutunza na kuuweka mkoa huo katika mazingira bora.
0 comments:
Post a Comment