Waandishi wawili wa
Zimbabwe wamekamatwa kuhusiana na ripoti ya gazeti moja ilioelezea
kwamba afya ya rais wa taifa hilo Robert Mugabe 'imedhoofika'
alipoelekea nchini Singapore kwa kile afisi ya rais huyo ilisema ni
zaira ya kimatibabu.
Muhariri wa gazeti la kibinafsi la NewsDay
,Wisdom Mudzungairi na mwandishi aliyeandika ripoti hiyo Richard Chidza
hatahivyo wameachiliwa na ni sharti wajiwasilishe mahakamani.Wakili wao Obey Shava amesema kuwa wameshtakiwa kwa kuhujumu na kutusi afisi ya rais.
Taarifa hiyo iliosema 'Mugabe yuko katika hali mbaya' ilinukuu duru zikisema kuwa rais huyo alisafirishwa kwa ndege siku ya Jumatano alfajiri.
- Mugabe: ''Naombewa nife''
- Mugabe: ''Nilikufa kisha nikafufuka''
- Mwanafunzi aliyempinga Mugabe akamatwa
- Mke wa Mugabe aamrishwa kurudisha nyumba tatu
Kulingana na chombo cha habari cha AP, watu wanaopatikana na hatia ya kumtusi Mugabe, uhudumia kifungo ijapokuwa kesi nyengine zimetupiliwa mbali.
0 comments:
Post a Comment