Na:Amiri kilagalila
Mkuu wa mkoa
wa Njombe CHRISTOPHER OLESENDEKA ameitaka jamii kuendelea kushirikiana ili
kuboresha kiwango cha taaluma kwa wanafunzi kwa kuwa matokeo na ufuhuru mzuri
hauwezi kuletwa na mtu mmoja.
Mkuu huyo wa
mkoa ametoa wito huo wakati wa mkutano wa umoja wa wakuu wa shule za sekondari
Tanzania (TAHOSA) mkoa wa Njombe uliofanyika katika shule ya secondary mpechi
halmashauri ya mji wa Njombe wenye lengo la kujadili masuala mbali mbali
yanayohusu elimu.
Afisa elimu
taaluma mkoa wa Njombe RAWLENCE MSELENGA amesema kuwa kwa mwaka 2016 mkoa wa
Njombe umeingia katika historia kubwa ya kufaulisha katika matokeo ya kidato
cha nne kitaifa kutokana na mikakati na juhudi miongoni mwa walimu hivyo kuto
kuludi nyuma katika kuboresha kiwango cha taaluma.
Licha ya
kufaulisha vizuri katika matokeo hayo ya kidato cha nne baadhi ya walimu
wamebainisha changamoto mbali mbali wanazokumbana nazo ikiwemo utoro kwa
wanafunzi na ubovu
Aidha kwa
pamoja wakuu hao wa shule wamewaomba wazazi kutoa ushirikiano katika uangalizi
wa watoto wao wanapokuwa majumbani na kuwaomba pia kuhamasika katika utoaji wa
michango ya chakula hususani shule za mijini ili kupunguza adha wanazokumbana
nazo wakati michango hiyo inapojitajika.
wa miundombinu.
0 comments:
Post a Comment