Msanii
wa filamu nchi Tanzania Wema Sepetu ametangaza rasmi kukihama Chama cha
Mapinduzi CCM na kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
Akizungumza
na waandishi wa habari leo akiwa ameambata na mama yake mzazi nyumbani
kwao Sinza Jijini Dar es Salaam, Wema amesema sababu kubwa ya kuhamia
CHADEMA ni ili kupata nafasi ya kupigania demokrasia anayodai kuwa
inapotea nchini Tanzania.
Sababu
nyingine aliyoieleza Wema ni kutelekezwa na CCM licha ya kujitolea
kutoa mchango wake kwa chama hicho wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa
mwaka 2015 kiasi cha kuwa hatarini kumwagiwa tindikali visiwani
Zanzibar.
"Kuanzia
sasa mimi siyo tena mwanachama wa CCM, na muda mfupi ujao nitachukua
kadi yangu ya CHADEMA... Nimeamua kuingia CHADEMA kwa sababu nataka
kupigania demokrasia, laiti ningejua, ningeingia zamani sana, najua
nimewahi kusema kuwa nitakufa nikiwa CCM, lakini sikujua kama itakuwa
hivi, laiti ningejua mapema basi nisingesema vile na ningejiunga CHADEMA
muda mrefu sana". Amesema Wema Sepetu
Amesisitiza
kuwa hajaamia CHADEMA kwa sababu ya pesa kama ambavo imekuwa ikidaiwa,
bali ni kwa ajili ya kupigania demokrasia, na kuweka wazi kuwa kuanzia
sasa ameingia kwenye mapambano ya kupigania demokrasia akiwa kwenye
chama ambacho anaamini kuwa ni chama peke chenye uwezo wa kurejesha
demokrasia inayopotea.
"Sijachukua
pesa yoyote kutoka CHADEMA, kama nimechukua hata shilingi 10,000 ya
CHADEMA basi kaburi la baba yangu huko Zanzibar litikisike" - Amesema Wema
Wema pia amejibu kuhusu baadhi ya wasanii kuidai CCm ambapo amesema "Ni kweli kuna madeni mengi wasanii tunaidai CCM, lakini kila wakati tukidai tunaambiwa tukamdai JK" - Wema Sepetu
Baada ya Wema kukabidhi kadi ya CCM, mama yake pia amerudisha kadi ya CCM na kusema "Tutatembea Tanzania nzima kuinadi CHADEMA". Kauli hiyo ilikuja baada ya mama huyo kueleza jinsi ambavyo CCM haikumtendea haki
Kuhusu sauti zilizosambazwa mitandani zikionesha Mama Wema akiongea na Steve Nyerere, mama Wema amesema "Kuhusu sauti zinazosemwa kuwa ni mimi na Steve Nyerere, siwezi kulizungumzia hilo maana sijazisikia"
0 comments:
Post a Comment