Na;Amiri kilagalila
Wamiliki,
watendaji na watoa huduma katika shughuli za utalii mkoani Njombe hususani
hoteli wameahidi kuongeza juhudi za utendaji kazi licha ya kuwepo kwa
changamoto mbali mbali ili kukuza sekta
ya utaliii katika mikoa ya nyanda za juu kusini.
baadhi ya wamiliki wa hoteli mkoani Njombe
wametoa kauli hiyo katika semina ya siku tatu ya mafunzo yenye lengo la kukuza
uchumi katika wizara ya mambo ya ndani yanayotekelezwa na mradi wa SPANIST na
kufanyika katika ukumbi wa halmashauri
ya wilaya ya Njombe.
Mkurugenzi
msaidizi wa mafunzo ya utafiti na takwimu idara ya utalii wizara ya mali asili
na utalii PASKASI MWIRY, amesema kuwa kwa sasa sekta ya utalii imekuwa ikifanya
kazi kwa kiwango cha chini kutokana na baadhi ya wamiliki wa hoteli kuwa na
watumishi wasiokuwa na vigezo sawia katika ufanyaji kazi.
Naye mratibu
wa SPANIST mikoa ya Nyanda za juu kusini GODWELL OLE MEING’ATAKI, amesema kuwa
lengo la kuendesha mafunzo hayo ni ktoa elimu kwa utoa huduma kutokana na
kuwepo kwa rasimali nyingi za asili katika mikoa ya kusini.
Aidha kwa
upande wake kaimu katibu tawala uchumi na uzalishaji mkoa wa Njombe LUSUNGU
MBEDE amesema kuwa yapo malalamiko mengi katika eneo la utalii kwa
wafanyabiashara hususani mlundikano wa kodi na kuahidi, kuwa serikali ya mkoa
wa Njombe mpaka sasa inalifanyia kazi suala hilo ili kufanya marekebisho katika
baadhi ya sehemu zinazolalamikiwa.
0 comments:
Post a Comment