internet advertising Waajili mkoani Njombe wametakiwa kuhakikisha wanalipa malimbikizo kwa wafanyakazi | DotFIVE

Waajili mkoani Njombe wametakiwa kuhakikisha wanalipa malimbikizo kwa wafanyakazi

Serikali mkoa wa Njombe imewataka waajili wote kuhakikisha wanalipa malimbikizo yote wanayodaiwa na wafanyakazi wao ili kuondokana malalamiko mbali mbali yanayofikishwa katika vyombo vya sheria.


Agizo hilo limetolewa na mkuu wa wilaya Njombe Ruth msafili kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Njombe CHRISTOPHER OLESENDEKA wakati alipo kuwa akifungua semina ya mafunzo kwa wanasheria,mahakimu, waendesha mashtaka pamoja na watumishi wa NSSF mkoani yenye lengo la kuboresha huduma za utoaji haki kwa jamii.

katika hatua nyingine mkuu  wa wilaya amesema kuwa baadhi ya mashirika ikiwemo NSSF yanakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo kutofikishiwa fedha kwa wakati huku mkoa wa Njombe waajili wakidaiwa na shirika lataifa la hifadhi ya jamii NSSF malimbikizo ya michango ya wafanyakazi wao inayofikia zaidi ya bilioni moja, ambayo ni fedha kubwa sana katika kukuza ustawi wa jamii.

    Baadhi ya wanasheria, mahakimu na watumishi wa NSSF wakisikiliza mafunzo

Kwa upande wake meneja wa NSSF mkoa wa Njombe ELINAMI MASAOE amesema kuwa shirika limekuwa na majukumu mbali mbali kitaifa ikiwa kutoa elimu dhidi ya uhifadhi wa jamii licha ya kuwepo kwa changamoto,hivyo litaendelea na majukumu hayo ili kuelewa dhana nzima ya hifadi ya jamii.

Kutokana na kuwepo idadi kubwa ya wafanyakazi katika makampuni mbali mbali kuwa na kesi nyingi mahakamani zinazotokana na waajili kushindwa kutekeleza wajibu wao, muwezeshaji wa semina hiyo kutoka makao makuu ya NSSF jijini Dar es salaam amesema kuwa upo utaratibu maalumu ambao mwajili hupewa miezi 6 ya matazamio kabla ya kufikishwa katika ngazi ya mahakama.


Kutokana na kuwepo idadi kubwa ya wafanyakazi katika makampuni mbali mbali kuwa na kesi nyingi mahakamani zinazotokana na waajili kushindwa kutekeleza wajibu wao, muwezeshaji wa semina hiyo kutoka makao makuu ya NSSF jijini Dar es salaam amesema kuwa upo utaratibu maalumu ambao mwajili hupewa miezi 6 ya matazamio kabla ya kufikishwa katika ngazi ya mahakama.
Share on Google Plus

About Amiri kilagalila

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment