internet advertising Njombe lazima ujengwe uwanja wa mpira wa kisasa | DotFIVE

Njombe lazima ujengwe uwanja wa mpira wa kisasa

    Christopher olesendeka
Na:Amiri kilagalila
"Tutaunganisha nguvu za wana Njombe wote ili tuhakikishe tunapata uwanja wa kisasa utakao tuingizia mapato mengi katika mkoa wetu"
Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher olesendeka ameahidi kuunganisha nguvu za Wananchi wa mkoa huo ili kujenga uwanja wa kisasa utakaofungua nafasi ya kuingiza mapato ya mkoa, Akizungumza wakati wa mapokezi ya timu ya Njombe mji baada ya kuifunga timu ya kurugenzi mjini Mafinga gori mbili kwa sifuri na kuiwezesha timu hiyo kufuzu kuingia ligi kuu.

Timu ya Njombe mji imepokelewa katika uwanja wa National housing mkoani Njombe  ambapo wanachi wengi wakionyesha furaha yao na kumuunga mkono mkuu huyo wa mkoa katika mapokezi mazito ya timu yao.

    Mashabiki na wananchi wakimsikiliza mkuu wa mkoa
Naye mkuu wa wilaya Njombe Ruth msafili ameonyesha furaha yake mbele ya wananchi kwa timu hiyo kufuzu kuingia ligi kuu na kuwaomba wanachi kuendelea kuonyesha uzalendo kwa kuinga mkono timu yao kwani nafasi hiyo ni ya pekee kwa sasa katika kujitengenezea kipato.

    Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth msafiri
kwa upande wake mwenyekiti wa timu hiyo Erasto mpete amesema kuwa wapo viongozi mbali mbali walioifanya timu hiyo kufikia mafanikio hayo licha ya kuwepo kwa viongozi wa mpira wa saliti ambao mda mwingine wamekuwa wakiludisha nyuma maendeleo ya timu, Mpete ametumia nafasi hiyo kuwataka makocha na viongozi wengine kuunganisha Nguvu kwani kwa sasa kilicho bakia ni umoja kwa kuwa timu imefikia hatua nzuri.

    Erasto mpete
Mashabiki wa mpira mkoa wa Njombe wameonyesha furaha na kuiombea timu yao huku badhi yao wakichangia timu hiyo mbele ya mkuu wa mkoa ambapo shabiki mmoja alitumia fursa hiyo kutoa fedha kiasi cha shiringi laki moja wakati mkuu wa mkoa akiahaidi laki moja kwa kila mchezaji.

   Wachezaji mbele ya mashabiki wakivalia taji la ushindi
Share on Google Plus

About Amiri kilagalila

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment